Korea Kaskazini yaifyatulia kombora Japan - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, July 28

Korea Kaskazini yaifyatulia kombora Japan


 

Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora, kulingana na maafisa wa Japan na Korea kusini.

Kombora hilo limeonekana likianguka katika bahari ya Japan kulingana na chombo cha habari cha kitaifa cha Japan.
Mapema mwezi Julai, Pyongyang ilidai kufanikiwa kulifanyia majaribio kombora la masafa marefu kwa mara ya kwanza.

Kombora hilo ni la hivi karibuni katika msururu wa makombora yaliofanyiwa majaribio hatua inayokiuka marufuku ya UN.

Umbali wa kombora hilo haujulikani.

Umbali wake umepingwa lakini wataalam wanasema kuwa linaweza kufika Alaska nchini Marekani.
Msemaji wa Pentagon Jeff Davis alisema kuwa kombora hilo lilirushwa na kwamba habari zaidi zinasubiriwa.

Kombora hilo la hivi karibuni ni la 14 kurushwa na Korea Kaskazini 2017.

Kombora hilo lilirishwa kutoka mkoa wa Jagang kaskazini mwa taifa hilo , kulingana na chombo cha habari cha Korea kusini Yonhap.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here