Senegal kupiga kura kwa kutumia leseni ya udereva - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, July 28

Senegal kupiga kura kwa kutumia leseni ya udereva


Mahakama kuu ya Senegal imepitisha ombi la rais Macky Sall kuruhusu wapiga kura kutumia pasipoti na leseni za udereva katika zoezi la kupiga kura.

.Kwa mujibu wa habari,Sall aliiomba mahakama siku ya Jumatatu kuwaruhusu wapiga kura wasiokuwa na vitambulisho kutumia pasipoti zao ama leseni kupiga kura.

Wapiga kura sasa wataweza kutumia pasipoti na leseni zao kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 30 mwezi Julai endapo watakuwa hawana vitambulisho maalumu vya kupiga kura.

.Hata hivyo upinzani umepinga kabisa umauzi huo na kusema kuwa umauzi huo unahatarisha  demokrasia nchini Senegal.

Muweka sheria wa Democratic party of Senegal PDS, Mamadou Lamine Diallo amesema kuwa si sheria wala sahihi kwa mahakama kupitisha suala kama hilo ndani ya miezi sita ya uchaguzi nchini humo.Amesema kuwa uamuzi huo hauendani na sheria ya ECOWAS.

Polisi walipiga mabomu ya machozi siku ya Alhamisi kutawanya wale wote waliokuwa wakipingana na sheria hiyo.


Senegal inatarajia kufanya uchaguzi wake siku ya Jumapil..

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here