Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Edina Deus anayedaiwa kutenda tukio hilo dhidi ya shangazi yake Rose Marwa (31) mkazi wa Bulubi
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alifanya hivyo baada ya kufokewa na shangazi kwa kosa la kukojoa kitandani wakati wamelala ndipo ugomvi ukazuka na hatimaye Edina alikwenda kumkaba kwa nguvu shingoni majeruhi Bi. Rose hadi kutoa ulimi nje kisha akaung'ata mpaka ukakatika.
Inasemekana baada ya kutokea tukio hilo waliweza kujitokeza ndugu wa majeruhi na kuweza kumpatia huduma ya kwanza na kuamua kuficha tatizo hilo ili iwe siri lakini hali ilivyozidi kuwa mbaya ndipo walipoamua kutoa taarifa kituo cha polisi na kuanza kufanya ufuatiliaji wa haraka eneo la tukio na kufanikiwa kumkata mtuhumiwa.
Pamoja na hayo, DCP Msangi amesema kuwa polisi wapo katika mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani huku majeruhi akiendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali aliyolazwa na hali yake inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment