Watu 14 wapotea baada ya mgodi kuporomoka Ghana - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, July 5

Watu 14 wapotea baada ya mgodi kuporomoka Ghana


Watu 14 hawajulikani walipo baada ya mgodi mmoja wenye dhahabu maeneo ya mji wa Prestea kuporomoka katika kanda ya magharibi mwa Ghana .

Inasemekana kwamba watu hao walikuwa wanachimba dhahbu kinyume na sheria .

Watu 5 waliponea chupu chupu baada ya kufanikiwa kutoroka wakati tukio hilo likitokea .

Watu hao wengine 14 wanahofiwa kufariki kwani kumekuwa na juhudi za kuwatafuta kwa takriban masaa 48 lakini bila ya mafanikio.

Ghana ni nchi ya pili baada ya Afrika Kusini yenye uzalishaji mwingi zaidi barani Afrika wa dhahabu lakini changamoto kuu inayokumba sekta hiyo ni shughuli za uchimbaji madini hayo kinyume cha sheria .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here